VIDEO: Navy Kenzo (@NavyKenzo) – Behind the Scenes of KAMATIA (BTS)



 Screen Shot 2016-02-02 at 9.52.47 AM

Dakika 36 za Waziri Mkuu Majaliwa, sentensi ya ‘kutumbua majipu’ ilivyowafurahisha wabunge




Feb 5 2016 Bunge la 11 mkutano wa pili  liliendelea Dodoma na Hotuba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  ndio ikahitimisha kwa kutoa kikao hicho.  Moja ya kauli zilizowavutia wabunge wengi katika sentensi zake ni pale alipoahidi kuyatumbua Majipu ya watendaji kazi wote wazembe Serikalini.


Tayari nimekurahisishia kuipata hotuba yote kwa kukusogezea hapa chini




Rich Mavoko kayaandika haya maneno 65 kisha akamalizia ‘Tusidharauliane’



Ukiwa nnje inawezekana unaweza ona mchezo ni rahisi ila ukiwa ndani ya mchezo utajua ugumu wake kiukweli hatulali kwajili ya hii kitu natamani hata wewe unaetukanaga watu ungejua ugumu wa izi mambo ungeishia kuachia mdomo wazi sisi ni kati ya watu tunaosakamwa lakini bado tunajali uwepo wenu na kuwategemea ningependa kusema haya ni maisha ya kioo ila baada ya hapa uzee so lazima tulijue ilo… #tusidharuliane


Mavoko

VIDEO: Party ya Alikiba alivyoileta kwa mara ya kwanza video yake mpya ya ‘Lupela’





Alikiba ni mwimbaji staa wa bongofleva ambaye kwa siku kadhaa zilizopita amewafanya Watanzania wawe juujuu kusikilizia single yake mpya ya ‘Lupela‘ ambayo rasmi ameiachia jana usiku February 4 2016 kwenye party iliyofanyika kwenye hoteli iliyo pembeni mwa bahari ya hindi…. itazame hii video hapa chini.

TCRA Yatowa Semina kwa Waandishi wa Habari Kugundua Simu Feki Zanzibar

Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Innocent Mungy, akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kutambua Simu Feki na kudhibiti uingiaji wa Simu hizo Tanzania na kueleza mwisho wa matumizi wa simu hizo Nchini Tanzania ni Juni 2016. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilima Zanzibar na kuwashirikisha waandishi wa Vyombo mbali mbali vilioko Zanzibar. 
 
 
 
 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano  TCRA Thadayo Ringo, akizungumza na waandishi wa habari jinsi ya kutambua Simu feki wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar, Amesema utambuzi wa kujua simu yako kama ni orijinali  unaweza kupiga namba kuaza na Nyota Reli 06 Reli . *# 06#  na utapata ujumbe wa Simu yako kwa Mfano zitakuja tarakimu 15  mfano   IMEI 12456789067654  Na Kupiga 15090 Ujumbe wa kukuelewesha kama ni simu yako orijino. kwa mfano kama huu Sony Mobile Communications AB -SONY  C5555 – Xperia. huu ni mfano wa kujua simu orijino.
 
 
 
 Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Thadayo Ringo akionesha mfano wa simu orijino kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
 
 
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
 
 
Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar.
 
 
Waandishi wakifuatilia mafunzo hayo kwa vitendo kuangalia somu zao kama ni orijino baada ya kupata elimu hiyo ya kujua simu feki na orijino wakati wa mkutano huo na Maofisa wa TCRA uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya zanzibar ocean view kilimani zanzibar. kwa kuingiza namba waliopewa.
 
 
Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya TCRA Innocent Mungy, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari baada ya kuangalia simu zao baada ya kuingiza namba hizo na kugunduwa kuwa ziko salama na siyo feki. kwa bahati nzuri takribani waandishi wote simu zao orijino.
 
 
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Watumiaji Huduma za Maweasiliano Thadayo Ringo akimsomea ujumbe mmoja wa waandishi wa habari aliyehudhuria mkutano huo baada ya kuweka namba hizo na kuja ujumbe wa suimu siyo feki.
 
 
Mdau wa habari Farouk Karim akiuliza swali wakati wa mkutano huo kuhusiana na uingiaji wa simu za kutoka ulaya nyingi huwa na lock wakati wa mkutano huo.
 
 
Mwandishi Amour Mussa akiuliza kuhusu TCRA inachukua hatua gani endapo simu ikiibiwa. 


Ndg Issa Yussuf akuliza jinsi ya utaratibu wa kuwafikia Wananchi wa Vijiji na zoezi hilo la ungunduzi wa simu feki na kuweza kuepuka na hasara hii, wakati ikifika tarehe hiyo ya mwisho wa matumizi ya simu hizo feki. 
 
 
Naibu Mkurugenzi Thadayo Ringo akifafanua na kujibu maswali yalioulizwa wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na matumizi ya Simu feki kufikia mwisho wake wa matumizi Tanzania.
 
 
Meneja Mawasiliano TCRA  Innocent Mungy  akifafanua jambo wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari Zanzibar kuhusiana na kusitishwa kwa matumizi ya simu feki ifikapo mwezi juni 2016. 
 
 
Kaimu Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Zanzibar TCRA Ndg Seif  S Waziri akizungumza wakati wa mkutano huo na kutowa neno la shukrani kwa waandishi wa habari kuhudhuria mkutano huo wa kutowa elimu ya simu feki kwa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Zanzibar  

Ray C kayaandika haya baada ya kuhusishwa tena na matumizi ya ‘Unga’







Msanii wa Bongo fleva Ray C leo ameonyeshwa kukwazwa na moja ya habari zilizoandikwa kenye moja ya kurasa za magazeti Bongo, na hiki ndicho alichokiandika.

 
ujingaaaaaaaaa

Seriously kwa kweli huwa naumia sana sana kuona binadam mwezangu anadiriki kuniharibia jina langu ilj yeye apate kula!hamjui mnaniathiri kiasi gani na hizi habari zenu?Hivi unadirikije kuandika usengwile kama huu bila hata aibu wala picha ya kuisapoti hiyo habari yani ni ujinga ujinga tu umeunganishwa na picha yangu bila hata uoga mmeichukua kutoka kwwnye page yangu ya insta bassss tayari mmeshapata story ili mradi tu mniharibie maisha yangu ili nyie mpate pesa mi nife maskini!!!kama kweli mnauhakika na mlichoandika kwanini hamkuweka picha yangu nikivuta hayp maunga badala yake mnaweka picha ya kituo cha mkunguni ambapo madaladala husimamisha kituoni hapo.mmepiga picha ya kituo cha mkunguni mkaona haitoshi mkaingia kwwnyw page yangu ya insta na kuchukua picha yangu niliojipiga mwenyewe ndio mnazitumia kunichafulia jina langu tena wakati ndio kwanza nahangaika kurudi tena kwenye kazi yangu.
Haki amungu sijawahi kuskia hata siku moja nyie global mmeandika kuhuau foundation yangu na mambo mazuri iliofanya,jw mnajua kama mpaka sasa nimeshatoa vijana zaid ya sabini kwenye madawa na wako fit wanatumia methadone je mnajua hilo?Hata siju moja sikawahi pata msaada wowote kutoka kwenu japo kunichangia nauli. tu ya kuja kwenye dawa kila siku hakuna hata anaenisaidia huu mwaka wa tatu bado naendelea kunywa dawa na ni kila siku ya mungu siku saba kwa wiki hakuna sikukuu wala msiba na ukikosa mwili unauma vibaya sana yani its not easy but am a fucking hard working woman na ni mwanamke jasiri napambana na siogopi kujaribu,naparangana na haya madawa na nayapinga na kamwe sintorudi nyuma na hizi nuksi mzipeleke kwenye familia zenu,wewe shigongo unamkosea sana mungu!unajifanya mlokolw lakini kazi yako ni kuharibia maisha ya wenzio unasahau kuwa malipl ni hapahapa duniani!Mimi ni kapuku tu sina mbwlw wala nyuma mbele yako lakini bado unanichimbia kaburi angali mi mzima.Na wewe 
Mayasa Marwata ni mpuuzi usie jua kazi yako!nimeisoma stori yako nimegundua ni mvivu Wa kufatilia habari!eti Chimbo LA unga langu lajulikana sasa kama ushalijua mbona haukunipiga nikivuta huo unga unaenda kupiga pixha kituo cha daladala bwege we!
Ntapambana na nyie MAHAKAMANI.”

CONFIRMED: Picha 4 za mfano wa gari la kifahari Diamond Platnumz analotaka kulinunua mwaka 2016


Mwimbaji kutoka kwenye muziki wa bongofleva Diamond Platnumz alikaa kwenye Exclusive Interview ya onAIRwithMillardAyo na kuzungumza vitu vingi sana kuhusu maisha yake na muziki wake ambapo moja ya maswali aliyoyajibu kwa kujiachia na akiwa ana tabasamu ni kuhusu kununua gari la ndoto yake.

Platnumz alimwambia Millard Ayo >>> ‘Nataka nibadilishe aina ya gari sababu imekua ni muda mrefu, nafikiri ni muda wa kuwa na gari nililokua nalitamani siku zote, gari la ndoto yangu ni Rolls royce na ndio ninalotaka kulinunua mwaka huu wa 2016 na litakua na jina la PLATNUMZ na sio namba za kawaida’

‘Mbali na kuwa msanii nimeshakuwa C.E.O sasa na kuna baadhi ya vikao ukija na gari ya kitoto huwezi kufanya dili vizuri, kuna baadhi ya sehemu siwezi kwenda naendesha mimi… pia siwezi kuendeshwa nikiwa nimekaa kwenye X6 naonekana kama muhuni tu… ndio maana nikipata Rolls royce inatengeneza heshima‘ – Diamond


 R2

Picha zote hizi ni mfano wa aina ya gari analotaka kulinunua Diamond Platnumz











































R4







R1