Picha na Kelvin Lameck |
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeongeza siku nne zaidi za
kujiandikisha kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura kwa Mkoa Dar es
Salaam.
Uamuzi huo umechukuliwa ili kukidhi mahitaji ya kuandikisha watu wote wenye sifa.
Awali,
uandikishaji ulitarajia kumalizika leo, lakini kutokana na nyongeza ya
siku hizo, sasa kazi hiyo itafikia tamati Agosti 4.
Mwenyekiti
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva alisema
Tume imefikia uamuzi huo baada ya kuona watu wengi wakiendelea
kujitokeza kujiandikisha, huku pia muda uliopangwa ukikaribia
kumalizika.
“Watu wengi wamejitokeza na kwa jinsi hali ilivyo, tumeona ni vizuri tukaongeza muda hadi Agosti nne,” alisema Jaji Lubuva.
Alisema
NEC imezingatia hali halisi ilivyo kutokana na mlundikano wa mambo kama
utoaji wa fomu za urais, uteuzi, wingi wa watu jijini na kuona ni vyema
kuongeza muda wa uandikishaji.
No comments:
Post a Comment